Idris Asema Wema Kutumia Tsh Milioni 4.8 kwa Ajili ya Nywele kwa Mwezi ni Hadhi yake


Baada ya mashabiki na wadau mbalimbali kujadili kauli ya Wema Sepetu ya kwamba anatumia Tsh 4.8 kwa ajili ya nywele zake kwa mwezi mmoja, mpenzi wake Idris Sultan amesema matumizi hayo yanaendana na hadhi ya mrembo huyo.

Aidha katika kauli nyingine ambayo Wema aliitoa mapema mwaka huu, alisema anatumia Sh 30,000 kwa ajili ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Idris Sultan ambaye ni mshindi wa shindano la Big Brother 2014, amesema haoni tatizo kwa mpenzi wake huyo kuwa namataumizi makubwa kwa kuwa yeye mwenyewe ni mtafutaji.

“Kwa level yake anafaa, kila mtu na level yake,” alisema Idris. “Kwa hiyo nina maanisha kila mtu ana thamani yake, na kila siku hadhi ya maisha yake inapanda na pia anafanya kazi ndiyo maana anafikia katika level hiyo,”

Pia Idris alisema watu wanatakiwa kutambua kwamba jinsi uchumi wa mtu binafsi unavyokuwa basi pia na maisha yake hudabilika pamoja na muonekano.
Previous
Next Post »