Akizungumza na waandishi wa habari katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kushushwa kwa mabasi hayo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya UDART, inayoendesha mradi huo, Charles Newe alisema ujio wa mabasi hayo ni neema kwa Watanzania kwa kuwa licha ya kuongeza ajira, lakini pia yatasaidia kuondoa changamoto ya upungufu wa mabasi.
Alisema kuwa mabasi hayo yanayotarajiwa kuanza kazi rasmi baadaye wiki ijayo na kuongeza idadi ya mabasi kuwa 210. Alisema, kwa sasa mabasi yaliyopo yanasafirisha abiria 200,000 kwa siku na kuwa kwa uwepo wa mabasi hayo mapya, idadi kubwa ya abiria zaidi itasafirishwa na kwa ufanisi zaidi. Newe alisema kwa sasa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu usafirishaji abiria kwa kuwa mabasi ni machache huku idadi ikiwa inaongezeka.
“Leo tumeshusha mabasi 70 ambayo ni imani yangu kuwa yakitunzwa vizuri, yataongeza ufanisi kwenye usafiri na kuwahudumia abiria wengi zaidi, sisi tunasafirisha watu hadi laki mbili kwa siku moja hasa zile siku za kazi, sasa ujio wa mabasi haya utatuongezea zaidi ufanisi wa kazi zetu,” alisema.
Thamani ya basi moja kati ya hayo yaliyoletwa jana ni Dola za Marekani 260,000, ambapo kwa mujibu wa Newe yatasaidia pia kuongeza pato la serikali kwa njia ya kodi. Mradi huo wa mabasi ya mwendokasi ulianza rasmi Mei 2016, ambapo unahudumia ‘ruti’ za Kimara kwenda Feri, Kimara hadi Gerezani, Gerezani hadi Morocco, Feri hadi Morocco, Gerezani hadi Muhimbili na Feri hadi Muhimbili. Hata hivyo, ‘ruti’ za Moroco kwenda Kariakoo na Posta zimekuwa zikikabiliwa na changamoto kadhaa, zinazokwamisha
ConversionConversion EmoticonEmoticon