BUNGE LAOMBWA KUTUNGA SHERIA ITAKAYOKUWA LAZIMA KUPIMA UKIMWI


Baraza la watu watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Katika halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe wameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kutunga Sheria itakayopelekea watu kupima Ukimwi kwa lazima.

Hayo yamesemwa na watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Konga ya Mbozi wakati walipotembelewa na Kamati ya Bunge ya Ukimwi ambayo ipo ziarani mkoani humo.

Wamesema  kuwa hatua hiyo itasaidia kwenye Mapambano ya Maambukizi na kuenea kwa ugonjwa huo ili kutimiza azma ya serikali ya 0.0.0 kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 hakuna Maambukizi Mapya ya Ukimwi.

Mmoja wa Waathirika hao Stephan Jonas alisema njia ya Mbadada ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni kuweka sheria ya kulazimisha kila kaya kupima ugonjwa huo.

"hili  suala inatakiwa liwe la lazima kwa sababu watu hawapimi, wanashindwa kujitambua hivyo wanaendelea kueneza kwa wengine sheria ikiwepo kila mtu apime kwa lazima itasaidia sana," alisema 

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge, Dr Jasmini Bunga alikubalina na Ombi hilo na kueleza kuwa litasaidia mkakati wa serikali wa kukabiliana na Maambukizi mapya ya Ukimwi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la JSI linashughulika na Mifumo ya maisha na Ustawi wa  Jamii Dr. Tulia Tuhuma alisema shirika lake litaendelea kufuatilia maendeleo ya Konga (Vikundi vya watu wanaoishi na Virusi vya ukimwi) pamoja na kusaidia utoaji wa huduma ya Ukimwi.
Previous
Next Post »