JINSI YA KUPAKA MAKE UP USONI.

JINSI YA KUPAKA MAKE UP USONI.

Tunapenda sana urembo hasa wa uso lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kupendezesha uso wako na kuonekana unavutia zaidi popote utakapotokelezea na watu wakasema waoohh you look gorgeous.
Sasa leo nimekuja na TIPS chanche za kukufanya wewe uonekane mrembo zaidi kila wakati .


1. USO -
osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na sabuni. kausha vzuri na kitaulo laini.
kama unatumia cleanser yoyote ni vizuri zaidi kuondoa uchafu kwenye uso wako kwa kutumia pamba na baada ya hapo osha tena uso wako kwa maji tuu ya uvuguvugu na ujikaushe.

2. FOUNDATION
Chagua faoundation inayoendana na rangi ya ngozi yako,

foundation ndo ya kwanza kupaka usoni kwako ili kuziba vidoa doa vilivyo kwenye ngozi ya uso wako ,paka kwa kutumia brush maalum ukianzia katikati kwenda chini na juu.epuka kuanzia kwenye pji la uso yani nywele zinapoanzia kwani itasbabisha mlundikano.


3. POWDER
Paka powder inayoendana na ngozi yako juu ya foundation,hakikisha unasambaza uso wako wote pamoja na sehemu za shingo ili rangi iwe sawa na uso. kwa kutumia spounge au brush inayohusika.
4MACHO
.uso wako ukiwa tayari ,andaa vifaa kwa ajili ya macho yako na nysi zako ambazo zitakua tayari zimechongwa vizuri,hapa inahitajika wanja brown/ mweusi ,eyeliner na eye shadows chagua rangi ianyoendana na ngozi yako au inayoendana na nguo utakazovaa ili kuleta maana.

chora vizuri nyusi zako kwa wanja wa brown , na upake eyeliner juu ya kope zako ili kuzipa rangi,then ndo unakuja kuweka eyeshadows ,ni vizuri kupaka eyeshadow za unga kuliko za maji .yani namaanisha kavu au za vumbi.

5.LIPS 
kama ni mpenzi wa lipstic za mafuta anza kwa kupaka lipshine ili uweze kulainisha lips zako then paka lipstick yako kulingana na rangi ulioichagua then paka na lipliner pembezoni mwa lips zako ili kuwekea ukingo.na kama ni mpenzi wa lipstick kavu haina haja ya kupaka lipshine paka lipliner yako then paka lipstick yako rangi uipendayo .


 y
LIPSTICK KAVU .
Baadaa kufuata hatua hizo tano hapo juu mdau wangu utakua tayari kwa mtoko wako .

ZINGATIO
Katika upakaji wa foundation na Powder unatakiwa uzingatie mda sababu kuna foundation nyingine ni kwa ajili ya mchana na nyingine ni kwaajili ya mitoko ya usiku hivyo basi ni muhimu kuzingatia na kuwa na make up ya mchana  na ya usiku kuepuka mchanganyiko.
NB  baada ya kumaliza shughuli zako hakikisha hulali na makeup yani wakati wa kulala hakikisha unanawa uso wako vizuri au unaweza futa kwa kutumia make up removal.
Previous
Next Post »