Waziri wa Nishati Dokta Medard Kalemani ameliagiza shirika la umeme nchini - TANESCO kuhakikisha linaongeza mashine mbili za kufua umeme katika kituo cha Mpanda Mkoani Katavi ili kuwa na umeme wa ziada kwa ajili ya kujiandaa na wawekezaji wa ndani na nje katika sekta ya viwanda.
Dokta Kalemani ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea mashine za mradi wa kufua umeme wa Orion utakaowezesha baadhi ya vijiji kupata umeme wakati wote wanapohitaji.
Amesema kutokana na kuanza kupelekwa kwa umeme huo katika vijiji vyote mkoa utahitaji mashine nyingine mbili kuvutia wawekezaji mkoa wa Katavi watakaoanza kunufaika na ongezeko la wawekezaji.
Akizungumza na wananchi wa Inyonga na vitongoji yake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Raphaeli Muhuga amewataka wananchi kujitoa kuwekeza katika sekta ya umeme.
ConversionConversion EmoticonEmoticon