VAA HERENI KULINGANA NA UMBO LAKO ILI UVUTIE ZAIDI

Ukiwa mrembo fauta ushauri, ili kwenda sawa ukitaka kujiweka katika hali ya kuvutia ni jambo la kawaida kwa mrembo au mtu yeyote anayeelewa maswahala ya mitindo ya kunakshi vazi lake linapokua limekamilika.

kwa vitu kama mikanda mikoba vibanio vya nywele, hereni,hata cheni,hutumika katika kupamba vazi la mtu husika

Katika makala ya leo utaweza kufahamu jinsi hereni zinavyoweza kutumika kupamba vazi lako.
Wanawake wengi kwa sasa wamekuwa wakitumia hereni kupamba mavazi yao. Pamoja na ukweli huo ni wachache kati yao wanaoelewa namna sahihi ya kuvaa pambo hilo.
Mara kadhaa jambo hili limekuwa likisababisha kuharibika kwa mwonekano wa mhusika, wakati mwingine kushindwa kupata ujumbe kamili kutoka katika mavazi waliyovaa.
Kwa mfano; ukiacha uvaaji wa hereni za madini ya fedha na dhahabu, wanawake wengi wamekuwa wakitumia hereni za rangi kunakshi mavazi yao. Hili siyo wazo baya.
Lakini, tatizo hutokea pale mvaaji anaposhindwa kutambua ni mtindo upi wa hereni unaoendana na umbo lake, au vazi alilovaa na hapa ndipo mkanganyiko unapotokea.
Hiyo ndiyo sababu iliyowahamasisha wadau wa mambo ya mitindo kubuni dondoo muhimu za uvaaji wa hereni ikiwa ni moja ya mapambo muhimu kwa mwanamke.
Kuzingatia maumbo ni moja ya mambo muhimu katika fani ya urembo, kwani kwa kulijua vyema umbo lako, utaweza kujua au kujifunza; ni aina gani ya vitu vinavyoendana na mwili wako.
Katika uvaaji wa hereni, warembo wengi wamekuwa wakifanya makosa makubwa bila ya wao kujitambua na kuharibu mwonekano wao, ingawa wanaweza kuwa katika mavazi ya kuvutia na ya gharama.
Ukiwa mrembo, fuata ushauri ufuatao ili kwenda sawa ukitaka kujiweka katika hali ya kuvutia:
• Ukiwa mwembamba na mwenye shingo ndefu unashariwa kutumia hereni kubwa au za kuning’inia, lakini zisiwe na marembo manene kama vile madungu.
• Ukiwa mwembamba na mwenye shingo fupi hereni za kuning’inia zitakupendeza, lakini ziwe nyembamba zenye umbo la mkufu na siyo za ringi, wala za madungu.
• Kama wewe ni mnene lakini una shingo ndefu, vaa hereni kubwa za kuning’ini zaweza kuwa za madungu au ringi kubwa; au umbo lolote kubwa na utavutia.
• Ikiwa wewe ni mnene lakini una shingo fupi, unashauriwa kuvaa hereni za kupachika fupi kama vile za skrubu, lakini zinapendeza zaidi zikiwa kubwa ili kuendana na umbo lako.
• Ukiwa mwembamba mfupi, vaa hereni ndogo za aina yeyote, ziwe za kupachika au za kuning’inia, zitakufanya uvutie zaidi.
• Kwa hereni za dhahabu au fedha, unaweza kuvaa na nguo ya aina yeyote .
• Kwa hereni za aina nyingine ni vizuri kuzingatia rangi ya nguo zako ili zilingane na kuonekana wa kisasa zaidi.

SOURCE
 NI MWANANCHI
Newest
Previous
Next Post »