BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), imedhamiria kusaidia upatikanaji wa masoko ili kuongeza mapinduzi yenye tija katika sekta ya kilimo nchini. Aidha imesema kuwa imelenga kuleta mabadiliko ya kilimo kutoka kwenye cha kujikimu kufikia kilimo cha kibiashara, ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Akizungumzia katika warsha ya kitaifa ya wadau ya sekta ya kilimo inayofanyika Dar es Salaam yenye mada kuu ya “Wazalishaji Tuanze na Soko, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas Samkyi, alisema ukosefu wa masoko ya mazao unaowakabili wakulima ni moja ya changamoto kuu zinazorudisha nyuma maendeleo ya kilimo nchini.
Samkyi alisema, ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na nyinginezo, Serikali iliamua kuanzisha TADB kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta ya kilimo.
“Katika kutekeleza majukumu yetu, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania,” alisema Samkyi.
Kwa mujibu wa Samkyi, benki hiyo inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi na kuongeza thamani.
Mikopo mingine ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi kupunguza upotevu wa mazao.
“Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani kuanzia uandaaji wa shamba hadi upatikanaji wa masoko, alisema. Aliongeza kuwa, wamejipanga kutoa mikopo ya ununuzi wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa madaraja ya mahindi na mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao, ikiwamo fedha za kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya mazao.
Akizungumzia mikopo itolewayo na benki hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo, Robert Pascal alisema, benki hiyo inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni ya muda mfupi usiozidi miaka miwili, mikopo ya muda wa kati ya miaka miwili hadi mitano, na mikopo ya muda mrefu.
Marejesho yanaeleweka kuwa ni kati ya miezi 60 hadi 180. Aliongeza kuwa, riba inayotozwa kwa upande wa mikopo ya muda mfupi ni asilimia saba mpaka nane kwa mwaka, ambayo mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kilimo kwenye mnyororo wa thamani.

ConversionConversion EmoticonEmoticon