KAMATI ya Kudumu ya Bunge Hesabu za Serikali (PAC) imempongeza Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omari Issa kwa kuwa mzalendo halisi aliyetumia njia ya gharama nafuu kununua magari 25 kwa bajeti ile ile, iliyotengwa ya kununua magari 11 yaliyokusudiwa.
Pongezi hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Felista Bura wakati kamati ilipokutana na kitengo hicho kujadili ripoti ya ukaguzi wa fedha wa taasisi hiyo.
Bura alisema hatua iliyochukuliwa na mtendaji huyo ni ya kizalendo na anastahili kupongezwa kwa sababu alitumia busara kufanya uchunguzi na kubaini fedha zilizotengwa kununua magari 11 zinatosha kununua magari 25.
“Kweli wewe ni mzalendo na ulitumia busara kwenye ununuzi wa magari hayo, ulinunua magari 25 kwa bajeti ile ile iliyoainishwa ya kununua magari 11,” alisema Bura ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM).
Awali akizungumzia jinsi alivyoweza kufanikisha ununuzi huo, Mtendaji huyo Issa alisema kitengo hicho kilipata fedha za msaada kutoka Benki ya Dunia kununua magari 11 aina ya Toyota Prado.
Ingawa hakutaja kiasi cha fedha kilichotolewa, lakini alibainisha kwamba walihitaji magari 11, ndipo wafadhili hao wakatoa fedha ambazo kama wangetumia mfumo wa manunuzi wa sheria ya serikali yangepatikana magari hayo 11

ConversionConversion EmoticonEmoticon