Mwakyembe: Usajili wa taasisi urekebishwe

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka mamlaka zote za Serikali zinazojihusisha na usajili wa taasisi za kijamii nchini kutafuta ufumbuzi wa haraka utakaorekebisha mfumo uliopo wa usajili wa taasisi hizo, ambao una kasoro nyingi.
Mamlaka hizo ni pamoja na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Wakala ya Usajili na Utoaji wa Leseni za Biashara (BRELA), Msajili wa Vyama vya Kijamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Sheria ya Usajili ya Vyama vya Ushirika.
Waziri huyo amebainisha kutokana na kasoro za mfumo huo wa usajili wa sasa matokeo yake kumekuwepo na utitiri wa taasisi za kiraia zikiwemo asasi za dini, asasi za kiraia na vyama vya ushirika ambazo baadhi yake zimekuwa zikitumia vibaya mianya ya Serikali kujinufaisha na kutimiza malengo yao bila kujali maslahi ya taifa.
Akizungumza katika kikao cha kazi na wakurugenzi wa mamlaka hizo Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe alisema kwa tathmini aliyoifanya amebaini mfumo uliopo wa usajili una kasoro kubwa ikiwemo kutokuwepo kwa mawasiliano katika kusajili miongoni mwa mamlaka hizo hali inayosababisha kuwepo kwa taasisi nyingi za kijamii zisizo na tija.
Dk Mwakyembe alisema kutokana na mfumo huo kwa sasa Tanzania ina utitiri wa asasi za kijamii zenye sifa na zisizo na sifa, zenye ofisi na zisizo na ofisi, zenye shughuli zinazoeleweka na zisizoeleweka zikiwemo taasisi za kijamii zinazoibuka pindi tu yanapotokea matukio makubwa kutokana na matakwa ya wafadhili wao.
Alisema atawasiliana na mawaziri husika wanaosimamia mamlaka hizo za usajili ili kwa pamoja waangalie namna ya kushughulikia tatizo hilo na kuja na ufumbuzi wa kudumu utakaodhibiti usajili wa kiholela wa taasisi za kijamii.
Tayari Dk Mwakyembe aliiagiza RITA kusitisha usajili wa taasisi yoyote ya kijamii hadi pale itakapohakiki idadi ya taasisi zilizosajiliwa chini yake na kutafutia ufumbuzi mfumo unaotumika wa usajili.
Previous
Next Post »

ConversionConversion EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng