HUJAMBO
MSOMAJI WA MAKALA YA AFYA YAKO AMBOKO UNAWEZA KUJUA MAMBO MBALIMBALI YAHUSUYO
AFYA NA KWA SIKU YA LEO NIMEKUANDALIA KUJUA UGONJWA WA MALARIA NIKUSIHI
Malaria ni ugonjwa wa kuambukizana unaoletwa na chembe chembe zinazoitwa plasmodium.Chembe chembe hizi huingia ndani ya mwili wa binadamu baada ya kuumwa na mbu wa kike kwa jina Anopheles. Mbu mwenye chembe chembe za plasmodium anapomuuma mtu,humuingizia baadhi ya mate yenye viini vya kuambukizana kwenye kidonda hivyo kusabaza Malaria. Viini hivi husafiri hadi kwenye maini ambapo hukaa hadi vifikie ukomavu. Viini hivi baadaye huingia na mtu kama huyu akiumwa na mbu,mbu huyu hubeba chembe chembe hizi na anaweza kumuambukiza mtu atakaye muuma.

Kuna aina 4 za Malaria: P. vivax, P. malariae, P. ovale na P. falciparum. Zimepewa majina kulingana na aina ya plasmodium inayozisababisha. Aina 3 za kwanza sio hatari lakini Falciparumni hatari sana na hata inaweza kusababisha kifo. Hii ni kwa sababu ikishaingia tu mwilini huzaana kwa wingi ndani ya damu.. Hii ni kwa sababu chembe chembe nyekundu za damu(ambazo husambaza oksijeni mwilini)zilizoadhirika huwa nzito na haziwezi kuingia kwenye kapilari. Hii husababisha kufa kwa sehemu ya ubongo,maini,mapafu,figo na matumbo kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni. Hali hii inaweza kusababisha kifo kama haita tibiwa haraka.
Baridi,kuuma kwa misuli na kichwa zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengi mengine. Njia ya pekee unayoweza kudhihirisha kama una Malaria ni kuenda hiospitalini kupimwa damu. Watu wengi wanaotoka sehemu zilizoadhirika na Malaria pindi wanapoona dalili hizi huenda kwenye maduka ya kuuza madawa kununua dawa za kupambana na Malaria. Huu sio ushauri mzuri. Ni muhimu kupimwa damu ili aina ya plasmodium inayosababisha maradhi yako itambulike na upewe matibabu yanayostahili.
MAKUNDI YALIYO
HATARINI KABISA KUPATA
Watoto wachanga,watoto na akina mama waja wazito wako kwenye hatarikubwa ya kushambuliwa hata kufa kutokana na Malaria. Watoto wachanga na watoto wako kwenye hatari kwa sababu wameambukizwa mara chache nahawajajenga
kinga dhidi ya chembechembe hiziVamizi la Malaria kwa wanawake wajawazito kalikwa sababu kinga yao dhidi ya maradhi huwa chini wakati wa uja uzito. Malaria huongeza tishio kwa mtoto ambaye hajazaliwa kama kuzaliwa kabla ya wakati
kutimia, uaviaji wa mimba, maambukizi ya sehemu za siri, uzani mdogo wa mtoto anapozaliwa, kupoteza uja uzito na pia ugonjwa huu unaweza kumsababishia mama kifo.

JINSI
YA KUJILINDA NA UGONJWA WA MALARIA
- Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa
Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na
Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
- Mbu wa
aina ya anopheles hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa
hivyo ni bora kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani
ya nyumba iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
- Kipindi
cha mwisho katika ukuaji wa mbu hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles
hupendelea maji yasiyo ya chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na
dawa sehemu zote ambazo mbu wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo
ama chochote ambacho kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti)
dawa asili ya kuua wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu
wachanga bila kuharibu maji.
- Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna
aina mbili ya neti hizi ambazo
zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa
kutibiwa kila baada ya miezi 6nba PowerTabs na zile zinazodumu kwa miaka 3
hadi 5 baada ya kutibiwa
Ni zipi dalili za Malaria?
Tiba ya Malaria
Tiba ya Malaria inategemea mambo kadhaa:
- Hali ya mgonjwa (mtoto, mama mja mzito, mtu mzima, ni kali ama
sio kali)
- Nguvu ya
dawa dhidi ya ambukizo la viini vya plasmodium.
- Eneo la
kijiografia ambalo mtu aliambukizwa. Kwa mfano, P.falciparuminayopatikana katika nchi za Mashariki ya kati inaweza kutibiwa
na dawa ya chloroquine, lakini inayopatikana Africa, katika nchi zilizo
kusini mwa jangwa la Sahara haitibiki kwa chloroquine.
- Aina ya plasmodium inayodhuru mgonjwa. Malaria yasiyo makali
hutibiwa na dawa za kumeza ilhali wagonjwa wenye P. falciparum kali hulazwa hospitalini na kupewa sindano ya
maji.
Msomaji
wa makala ya afya yako usikose makala nyingine ambayo utaweza kujua zaidi
magonjwa mbalimbali na kesho nitakuandalia makala itakayo husu ugonjwa wa
kifafa na namna ya kujikinga na pamoja
dalili zake usikose
ConversionConversion EmoticonEmoticon