Madaktari sita kutoka muungano wa madaktari nchini Kenya wamepewa hukumu ya kusimamishwa kazi kwa muda wa mwezi mmoja kwa kukataa kusitisha mgomo unaoendelea wa madaktari ambao umedhoofisha shughuli za matibabu katika serikali za umma, kwa mujibu wa taarifa za gazeti la Daily Nation.

Mahakama ya Ajira na mahusiano ya kazi nchini Kenya imeamuru muungano wa madaktari kusitisha mgomo huo na kumaliza mazungumzo na serikali katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Madaktari wa Kenya wanaogoma wakiwa katika mkutano wa kuangalia nini cha kufanya baada ya mahakama kuwaamuru wasitishe mgomo
Juhudi kadhaa za kumaliza mgomo huo zimegonga mwamba huku madaktari wakitaka kutekelezwa kikamilifu kwa mkataba uliosainiwa baina yao na serikali mwaka 2013 ili kuboreshwa kwa malipo na hali bora za kazi.
Jaji Hellen Wasilwa amesema kuwa iwapo maafisa watakaidi amri ya mahakama watafungwa jela wiki mbili. 
Previous
Next Post »