Hujambo msomaji wa mfululizo wa makala ya afya
inayokujia kila siku leo tutazungumzia ugonjwa wa fangasi amboaumekua tatizo
kwa watu wengi kwa wanawake pamoja na wanaume.
Kati ya
maambukizi yanayowasumbua wanawake wengi duniani ni maambukizi ya fangasi.
Inakisiwa asilimia 75 ya wanawake wote duniani hupata maambukizi haya katika
kipindi cha uhai wao.
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za
mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida
albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush.
Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha
chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na
hata kwenye uke.
Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja aina fulani za bakteria
wanaoishi pamoja na fangasi hawa husaidia sana katika kuthibiti maambukizi
yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi.
Nini hutokea?
Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na
sehemu nyingine (kama zilivyoelezewa hapo juu) bila kusababisha madhara yoyote
yale isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika kama vile
mabadiliko katika hali ya pH ya eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida
ndani ya uke ni 4.0 - 4.5) au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine
unapoharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina
ya antibiotics, kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.
Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu
kuu mbili;
1. Maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated thrush:
Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi mara moja hadi nne kwa mwaka
na dalili zake huwa si mbaya sana na maambukizi haya husababishwa na fangasi wa
jamii hii ya Candida albicans.
2. Maambukizi makali yaani complicated thrush: Katika kundi
hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi zaidi ya mara nne kwa mwaka, dalili zake
kuwa mbaya zaidi au kama maambukizi yatakuwa yametokea kipindi cha ujauzito,
ugonjwa wa kisukari, upungufu wa kinga mwilini. Aina hii kusababishwa na
vimelea vya aina nyingine tofauti na Candida albicans.
Vihatarishi
Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi
hawa ni wale wenye;
• Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri
au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji
yaliyochanganywa na siki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali husababisha
kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria
aina ya lactobacilli
• Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo
yana tabia ya kushusha kinga ya mwili
• Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambayo husababisha
mabadiliko katika s ehemu za siri na hivyo kufanya kuwepo kwa ukuaji wa kasi wa
fangasi hawa
• Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini
na kupungua kwa kinga ya mwili). Hata hivyo ieleweke hapa kuwa si kila mjamzito
hupatwa na maambukizi haya.
• Matumizi ya dawa za kupanga uzazi (vidonge vya majira)
• Upungufu wa kinga mwilini kutokana na magonjwa sugu kama
kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya mononucleosis na nk.
• Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS)
• Matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana
na sababu mbalimbali
• Matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo
ya uzazi (infertility treatment)
• Msongo wa mawazo (stress)
• Utapia mlo (malnutrition)
• Kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri
kwa muda mrefu kama nguo za kuogelea (swimwear), nguo za ndani zilizotengenezwa
kwa kitambaa aina ya nylon, nguo za ndani zinazobana sana nk.
• Kuvimba kwa tezi la koo (goiter)
• Saratani ya tezi la koo (thyroid cancer)
• Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na
thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao
wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako
kwenye hatari kubwa.
Kwa wanaume vihatarishi vya maambukizi haya ni;
• Kujamiana na mwanamke mwenye tatizo hili au maambukizi
haya
• Upungufu wa kinga mwilini
• Matumizi ya madawa aina ya antibiotics kwa muda mrefu bila
ushauri wa daktari
• Magonjwa sugu kama kisukari, saratani ya aina yoyote ile
na nk.
Dalili na viashiria kwa wanawake;
• Kuwashwa sehemu za siri
• Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)
• Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness)
• Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia)
• Maumivu au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo
(wakati mtu anakojoa)
• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa mdomo wa nje wa tupu ya
mwanamke (labia minora)
• Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu,
unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini (cottage
cheese like discharge) wenye muonekano unaojulikana pia kama curd-like
appearance. Kwa kawaida, uchafu huu haumbatani na harufu yoyote isipokuwa
panapokuwa na tatizo la ziada kama ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria
vaginosis. Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine
yaliyokaribu na tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki (groin area) au perineum
na kusababisha kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.
Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi wakati mwanamke
anapokaribia kupata hedhi.
Dalili na viashiria kwa wanaume ni;
• Kuwashwa sehemu za siri
• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye ncha ya uume
• Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama nilivyoeleza hapo
juu) kwenye sehemu ya juu ya uume.
• Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore on the glans)
Hata hivyo, mara nyingi wanaume hawaoneshi dalili zozote
zile, ni vizuri kwa mwanamke kumueleza mwenza wake pale anapopata maambukizi
haya ili naye pia apate kutibiwa.
Vipimo vya uchunguzi
Kabla ya vipimo vya uchunguzi, ni muhimu kwa daktari
kuchukua historia ya mgonjwa kwa usahihi kabisa. Vipimo vitahusisha;
1. Kuchunguza uchafu unaotoka kwa kutumia hadubini
(microscope). Mara tu baada ya kuchukua sehemu ya uchafu kwa kutumia swab,
kipimo hicho humwagiwa tone la 10% potassium hydroxide ambayo huyeyusha
chembechembe za ngozi na kubakisha seli za Candida albicans. Kuwepo kwa pseudohyphae
(mfano wa aina fulani ya mizizi au miguu ya fangasi hawa) pamoja na budding
yeast cells (yaani seli za fangasi zinazojigawa kwa ajili ya kuzaliana) ni
uthibitisho wa maambukizi ya fangasi aina ya Candida albicans.
2. Kuchukua kipimo na kuotesha kwenye maabara ili kuangalia
aina ya uoto huo kama ni wa fangasi aina ya Candida albicans, ama la.
3. Kipimo cha mkojo (Urinalysis)
4. Vipimo vingine hufanyika kulingana na dalili
zinazoashiria uwepo wa magonjwa mengine kama vile ugonjwa wa kisukari,
HIV/AIDS, ugonjwa wa kuvimba tezi la koo (goiter), saratani ya tezi koo
(thyroid cancer) nk.
Matibabu
Matibabu ya fangasi huusisha dawa za kutibu fangasi (antifungal
drugs) kama vile dawa za kupaka za topical Clotrimazole, topical
Nystatin, Fluconazole au topical Ketoconazole.
Wagonjwa wenye maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated
va#@ginal candidiasis wanaweza kutumia dawa za kupaka (cream) kutoka
dawa za fangasi za jamii ya -azole kama vile Butoconozale,
Miconazole, Clotricomazole nk. Dawa hizi hutumika kwa muda wa siku 3-7
kulingana na aina ya dawa. Mgonjwa anashauriwa kupaka dawa ndani ya uke pamoja
na maeneo yote yanayozunguka sehemu hiyo. Jinsi ya kupaka dawa hizi ni kuanzia
mbele kuelekea nyuma.
Aidha mgonjwa anaweza kupewa dawa za kutumbukiza ukeni
ambayo atatumia kwa muda wa siku 3-14 kulingana na aina ya dawa. Dawa hizo ni
pamoja na Miconazole, Tiaconazole, Terconazole, Nystatin nk. Kidonge cha
kumeza aina ya fluconzole pia huweza kutolewa. Dawa hizi nilizotaja hapa
juu zina kawaida ya kuharibu ubora wa mipira ya kondomu zilizotengenezwa na
mpira aina ya latex (latex condoms) pamoja na vifaa vya upangaji uzazi
aina ya diaphragms. Ni vizuri kwa daktari kabla ya kumpa mgonjwa dawa hizi
kumfahamisha kwa ufasaha jinsi ya kuzitumia na tahadhari anayotakiwa mgonjwa
kuchukua. Inashauriwa kama baada ya matumizi haya bado mgonjwa ana dalili za
maambukizi au mgonjwa akapata tena maambukizi haya ndani ya miezi miwili baada ya
matibabu ya awali, basi anashauriwa kwenda kumuona daktari ili apate matibabu
zaidi.
Kwa wale wenye maambukizi makali yaani complicated
v@ginal candidiasis, kabla ya kupewa tiba, ni muhimu kwanza kufanyiwa
kipimo cha kuotesha sehemu ya uchafu unaootoka ukeni ili kuwa na uhakika kama
kweli fangasi wanaosababisha maambukizi haya ni Candida albicans ama la,
kwani fangasi aina ya Candida glabrata pia wanaweza kusababisha aina ya
maambukizi haya na huwa siyo rahisi kutibika kwa kutumia matibabu ya kawaida ya
kutibu fangasi pamoja na pia si rahisi kuonekana kwa kutumia hadubini
(microscope).
Matibabu ya wagonjwa wenye aina hii ya fangasi hujumuisha
matumizi ya dawa za kupaka au vidonge vya kuweka ukeni kwa muda mrefu yaani kwa
muda wa siku saba hadi kumi na nne (7-14) au dawa aina ya fluconazole
ambayo hutumika kila baada ya siku tatu (yaani siku ya 1, siku ya 4 na siku ya
7). Mara baada ya kumaliza tiba hii, mgonjwa hutakiwa kuendelea nayo mara moja
kwa wiki kwa muda wa miezi sita. Ikiwa matibabu haya hayatasaidia basi mgonjwa
anaweza kushauriwa kutumia mchanganyiko wa fluconazole pamoja na dawa ya kupaka
ya Clotrimazole mara mbili au moja kwa wiki kulingana na dozi ya dawa,
au fluconazole na dawa nyingine za kupaka kwa wakati mmoja.
Matibabu ya wagonjwa wenye maambukizi hatari sana yaani severe
v@#ginal candidiasis ambayo kwa kawaida huambatana na dalili kama uke kuwa
mwekundu sana, uke kuvimba, michubuko ya ngozi ya ukeni (excoriation) na
kutokea kwa mifereji kama vidonda (fissure formation) huwa ni dawa zozote za
kupaka zilizotajwa hapo juu kwa muda wa siku 7 mpaka 14 au dawa ya fluconazole
ambayo hutolewa mara mbili, ambapo dozi ya pili hutolewa siku ya tatu baada ya
kutolewa kwa dozi ya awali (second dose 72hrs after initial dose).
Matibabu ya maambukizi ya fangasi ambayo hayasababishwi na Candida
albicans kwa mfano Candida glabrata nk ni matumizi ya dawa za kupaka
jamii ya nonfluconazole azole groups kama vile Posaconazole,
Voriconazole nk zitolewazo kwa muda wa siku 7 mpaka 14 pamoja na kidonge
cha Boric acid kwa muda wa siku 14. Mtu mwenye maambukizi haya pia anashauriwa
kuonana na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama.
Kwa vile maambukizi ya fangasi hutokea sana kwa wanawake
wajawazito, hivyo basi wanashauriwa kutibiwa kwa kutumia dawa za kupaka tu kwa muda
wa siku 7. Aidha dawa aina ya Itraconazole haipaswi kutumiwa na mwanamke
mjazito au anayekusudia kushika mimba. Dawa ya Ketoconazole haipaswi
kutolewa bila ushauri wa daktari kwani ina madhara ya kusababisha ugonjwa
hatari wa Ini (Fulminant hepatitis). Usugu wa fangasi dhidi ya dawa za
jamii ya azole groups hutokea baada ya matumizi ya dawa za vidonge (vya
kumeza) za kutibu fangasi kwa muda mrefu.
Maambukizi ya fangasi pia huonekana sana kwa wagonjwa wenye
Ukimwi. Tiba ya maambukizi haya ni sawa na tiba ya watu ambao hawana ugonjwa wa
Ukimwi. Hata hivyo, kwa wale wagonjwa wa ukimwi ambao wamepata maambukizi ya
fangasi mara kwa mara wanashauriwa kunywa dawa aina ya fluconzole mara moja kwa
wiki kama kinga dhidi ya maambukizi haya au kama njia ya kupunguza fangasi
hawa. Kadhalika dawa za kutibu fangasi aina ya Itraconazole, Voriconazole,
Posaconazole huingiliana sana katika utendaji kazi na dawa za kurefusha
maisha za ugonjwa wa Ukimwi (Antiretroviral drugs, ARVs) aina ya Protease
Inhibitors, PIs (rotinavir nk.) na Nonnucleoside Reverse Trancriptase
Inhibitors, NNRTI (maraviroc nk).
Wakati mwingine, maambukizi ya fangasi yanaweza kuambatana
na magonjwa ya zinaa (Bacterial vaginosis nk), hivyo dawa zitatolewa
kulingana na dalili na historia ya mgonjwa.
Kinga ya maambukizi ya fangasi
• Kuosha sehemu ya siri kwa kutumia kitambaa kisafi kila
siku na kuosha kuanzia mbele kuelekea nyuma, epuka kurudia ukishafika nyuma.
• Epuka matumizi ya sabuni zenye manukato, bubble baths,
v@#ginal deodorant products, feminine hygiene, na bath powder.
• Vaa nguo za ndani ambazo hazibani sana na zilizotengenezwa kwa
kutumia pamba au hariri (silk), epuka synthetic underwear.
• Epuka mavazi yoyote ya kubana kama jeans za kubana nk.
• Badilisha nguo za ndani kila zinapopata unyevunyevu.
• Fua nguo za ndani zako kwa maji yenye nyuzi joto 90 na
kuendelea.
• Tumia pad wakati tu unapozihitaji (kama umeingia kwenye
mzunguko wako wa hedhi)
• Kula mlo wenye virutubisho vyote kamili (balanced diet)
• Epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako ambaye amepata
maambukizi ya fangasi.
• Epuka kuoga maji moto sana (hot baths) tumia maji ya
uvuguvugu, hii kwa wale ambao wanaishi kwenye ukanda wa joto (tropical
climate).
• Matumizi ya vifaa vya ngono , vifaa vya upangaji uzazi
(diaphragms, cervical caps) yanaweza kuleta kujirudia kwa maambukizi ya fangasi
kama havitaoshwa na kukaushwa vizuri baada ya kutumiwa.
• Baadhi ya tafiti zilizofanyika, zimethibitisha ya kwamba
unywaji wa maziwa ya mtindi (yoghurt) yenye live culture, husaidia kupunguza
maambukizi ya fangasi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon