Karibu mpenzi msomaji katika makala ya afya yako na hapa tunaangazia
magonjwa mbali mbali na kukumbushana pale tuliko jisahau kuhusu afya zetu leo tutaongelea ugonjwa wa kifua kikuu ambao ni tishio kubwa
Kifua kikuu (kwa Kiingereza tuberculosis, kifupi TB) ni ugonjwa wa
kuambukizwa ulio hatari. Ugonjwa huu husababishwa na aina mbalimbali za bakteria ambazo hujulikana kama Mycobacterium tuberculosis.
Kifua kikuu
husambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kupitia hewa wakati anapokohoa, kupiga chafya, aumate yake yakiwa hewani
Maambukizi
mengi hayana dalili wala hayaleti madhara. Lakini moja kati ya maambukizo kumi yasiyoleta
madhara hatimaye huendelea na kuwa ugonjwa kamili. Kama kifua kikuu
kisipotibiwa, kinaua zaidi ya 50% ya watu walioambukizwa.
Dalili za kifua kikukuu ni pamoja na kukohoa kwa wiki mara
mbili au mfululizo homa za mara kwa mara kwa wiki mbili au zaidi,kutokwa kwa
jasho jingi hasa kwa nyakati za usiku,kukohoa makohozi yenye damu, kupungua
uzito zaidi ya kilo 3 ndani ya wiki 4 au kukonda na kukosa hamu ya kula
Maambukizi
ya viungo vingine husababisha dalili mbalimbali. Njia ya kitaalamu ya utambuzi
wa kifua kikuu kwa kutumia eksirei ya kuchunguza ugonjwa hujulikana kama
eksirei ya kifua na pia wanatumiahadubini na kufanya uchunguzi wa vimelea
maradhi vya majimaji ya mwilini. Uchunguzi wa kifua kikuu
kisicholeta madhara hutumia kipimo kiitwacho kipimo
cha ngozi (TST) na vipimo vya damupamoja na Kifua kikuu
hugundulika kwa kupima makohozi na ikibidi x-ray na matibabu yake ni bure katika hospitali zote za serikali na
binafsi
Unapoona mtu ana dalili moja wapo kati ya hizi au wewe
mwenyewe mshauri awahi kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi tiba na
awasiliane na mratibu wa kifua kikuu
aliye karibu nae kwani mmoja huweza kuambukiza watu kati ya 10 hadi 15 kwa
mwaka kamam ajapata matibabu.wastani wa
watu 176 huugua kifua kikuu kila siku nchini Tanzania na wastani wa watu 12hufariki dunia kila siku
Ikitokea umegundulika kua unakifua kikuu usihofu kwani
kinatibika na mamilioni ya watu duniani kote wameugua na kupona. Unachotakiwa
kufanya ni kufatisha masharti utakayopewa na daktari kama; kunya dawa kila siku
kwa muda uliopangiwa ili kupona kabisa. Matibabu yake huchukua huchukua kati ya
miezi sita hadi minane
Endapoumegundulika na kifua ki kuu kumbuka kufunika mdomo na
pua unapo kohoa au kupiga chafya ili usiambukize watu wengine na pia usiteme
mate ovyo
Pumzika kiasi cha kutosha,kula chakula chakula bora na
uwafahamishe ndugu na marafiki kwamba
unaugua kifua kikuu na uko kwenye matibabu na ukisha kamilisha matibabu nenda
kwa uchunguzi ili kutibitisha kama
umepona.
Kumbuka ni muhimu kuendelea kutumia dawa mpaka mwisho hata
kama unajisikia vizuri ili usipate kifua kikuu sugu ambacho matibabu yake ni
magumu. Mara kwa mara kifua kikuu kimekuwa kikihusishwa na na ugonjwa wa ukimwi
kwani asilimia 50 ya watu wenye kifua kikuu wana VVU kama umethibitika unakifua kikuu ni
muhimu ukapata ushauri na saa na kupima virusi vya ukimwi,kwani asilimia 10-15
ya watu wanao ishi na VVU waugua kifua
kikuu hivyo ni muhimu kuchunguzwa kama
una kifua kikuu ili kuboresha na kuokoa maisha yako kwani kifua kikuu
kinatibika kabisa hata kama unamaambukizi ya VVU
Na pia ili
kuzuia kifua kikuu, ni lazima watu wapimwe ugonjwa na wapate chanjo ya bacillus Calmette - Guérin.
Wataalamu wanaamini kwamba theluthi moja ya idadi ya watu duniani waliambukizwa kifua kikuu, na kila sekundekuna mtu ambaye
anaambukizwa Mwaka 2007,
kadri ya watu 13,700,000 duniani waliambukizwa kifua kikuu kinacholeta madhara
sugu Mwaka 2010,
kadri ya milioni 8.8 ya watu waliambukizwa na milioni 1.5 ya watu walifariki
baada ya kuambukizwa na kifua kikuu, na wagonjwa wengi wanapatikana katika nchi
zinazoendelea Idadi halisi ya wagonjwa wa kifua kikuu
imekuwa ikipungua tangu mwaka 2006, na
kesi mpya zimeshuka tangu mwaka 2002
Kifua kikuu si ugonjwa
unaosambazwa sawasawa duniani kote. Kadri ya 80% ya watu katika nchi nyingi za Asia na Afrika waliofanyiwa kipimo
cha ngozi walionekana wameambukizwa, lakini ni asilimia 5-10% tu ya wananchi wa Marekani ambao walionekana na
ugonjwa huo. Watu wengi waliopo katika nchi
zilizoendelea wanaambukizwa
kifua kikuu kwa sababu ya kutokuwa na kinga. Kwa kawaida, hawa watu
wanaambukizwa kifua kikuu baada ya kuambukizwa na VVU na hatimaye wanapatwa
na UKIMWI.
TIBA
Kwa kawaida,
mgonjwa wa kifua kikuu anatumia vidonge kila siku wakati wa matibabu
yanayosimamiwa.
Ugonjwa wa kifua
kikuu kikali unaweza kutibiwa kwa mchanganyiko wa antibiotics. Mchanganyiko
sahihi wa dawa za kifua kikuu hutoa kinga na tiba.
Tiba inayofaa
humwezesha haraka mgonjwa wa kifua kikuu kutoambukiza na kwa hiyo huzuia kuenea
zaidi kwa kifua kikuu. Kufanikisha tiba ya TB, huchukua miezi sita hadi minane
ya matumizi ya dawa ya kila siku.
Dawa za aina
mbalimbali zinatakiwa kutibu kifua kikuu kikali. Kutumia dawa mbalimbali
kufanya kazi nzuri ya kuua bakteria wote na huenda ikakinga dhidi ya usugu kwa
dawa.
Dawa zinazotumika
zaidi ni Isoniazid, Rifampin (Rifadin, Rimactane), Ethambutol (Myambutol) na
Pyrazinamide.
Kuhakikisha
matibabu kamili, mara nyingi inapendekezwa kuwa mgonjwa ameze vidonge mbele ya
mtu atakayesimamia matibabu. Njia hii inajulikana kuwa DOTS (matibabu yanayofuatiliwa
moja kwa moja, muda mfupi). DOTS hutibu kifua kikuu kwa 95% ya wagonjwa.
ConversionConversion EmoticonEmoticon