MLIPUKO WA BOM WAUWA WATU 27 LIBYA

 Watu 27 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa karibu na msikiti mmoja katika mji wa Benghaz nchini Libya utokana na shambulio la kigaidi.Washambuliaji walitumia gari lenye vilipuzi kutekeleza mpango wao huo.
Milipuko hiyo miwili nje ya msikitiki karibu na eneo la Al Suleiman,ilitokea jioni katika swala ya maghari,ambapo waumini hao wakati wanatoka ndani ya msikiti ndipo walipolengwa na shambulio hilo.
Vipande vya picha za video zilizoonyeshwa kupitia Televishen ya taifa,zimeonesha miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo ikiwekwa ndani ya gari la Polisi.
Katika shambulizi hilo gari la kwanza lilifika wakati waumini wakitoka na kulipuka,ambapo gari la pili katika shambulizi hilo lililipuka muda mfupi upande wa pili wa mtaa huo dakika chache baadaye lililo beba vilupuziw
Wanajeshi pamoja na raia ni miongoni mwa watu waliathiriwa na shambulizi hilo.Hata hivyo idadi ya watu waliojeruhiwa na vifo huenda ikapanda kutokana na watu wengi kujeruhiwa.
Bado haijafahamika kwamba ni kundi gani lililoshiriki katika shambulizi,kwani hakuna ujumbe wowote uliotolewa kukiri kushiriki.
Mji wa Benghazi umekuwa kitovu cha machafuko kati ya wapiganaji na vikosi vya serikali.
Hata hivyo pamoja na kwamba Libya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mambomu,lakini milipuko miwili ndani ya dakika 15 ni jambo lisilo la kawaida
Taifa la Libya lilijikuta katika machafuko Zaidi, baada ya kuangushwa kwa utawala wa Muamma Gaddafi mwaka 2011,ambapo makundi yanayotaka kutwaa madaraka yakaibuka na hivyo kutoka mwanya wa kundi la kigaidi la Islamic state kuimariki nchini humo.
Previous
Next Post »