Viongozi wa Acacia wajiuzulu

Mkurugenzi Mkuu wa Acacia nchini Tanzania Brad Gordon na Mkurugenzi Mkuu wa fedha Andrew Wray, wamejiuzulu nyadhifa zao ingawa bado watakuwa chini ya kampuni mpaka mwisho wa mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa leo na kampuni hiyo na kusema kwamba Mkurugenzi Mkuu Brad Gordon anarejea nyumbani kwake Australia na Andrew Wray anatafuta fursa mahali kwengine.

Tayari Bodi ya Acacia imewataja watu ambao watachukua nyadhifa za wawili hao, ambao ni Peter Geleta ambaye atakuwa Mkurugenzi Mkuu na Jaco Maritz atakachukua nafasi ya Andrew Wray aliyekuwa Mkurugenzi wa fedha.
Peter ambaye ametajwa kuwa na uzoefu kwenye uchimbaji madini kwa muda wa miaka 35 ameshawahi kufanya kazi na mgodi wa Anglo Gold Ashanti kwa miaka 25 na kampuni ya Barrick, na alijiunga na Acacia mwaka 2012 na alishawahi kuwa Meneja Mkuu kwenye mgodi wa Bulyanhulu.

Acacia imewashukuru viongozi waliojiuzulu Brad Gordon na Andrew Wray kwa muda wao wote waliokuwa hapo huku wakisema walifanya nao kazi vizuri, na kuwatakia heri huko waendako, huku wakiamini waliochukua nafasi yao watafanya kazi kama ambavyo inastahili.
Previous
Next Post »