Hospitali za Rufaa za mikoa ya Kanda ya Ziwa zinakabiliwa na ukosefu wa mashine ya Viral Load,yenye uwezo wa kupima kiwango cha chembechembe za kinga za mwili (CD4) kwa mtu mwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi, hali ambayo inadaiwa kusababisha majibu ya vipimo hivyo kuchukua hadi miezi sita kupatikana na hivyo kuathiri tathmini ya maendeleo ya utumiaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi.
Afisa Tathimini na ufuatiliaji wa maambukizi ya ukosefu kutoka Baraza la Taifa la watu wanaoishi na ukimwi Tanzania ( NACOPHA ) Last Mlaki wakati wa ziara ya kamati ya kupambana na kuzuia maambukizi ya ukimwi ya halmashauri ya jiji la Mwanza, ilipotembelea mashirika yanayotekeleza miradi ya kudhibiti ukimwi katika jiji hilo ambapo wameelezea kuwa ni hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa ya Bugando pekee ambayo inamiliki mashine hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi katika halmashauri ya jiji la Mwanza, ambaye pia ni Naibu Meya wa jiji hilo Bhiku Kotecha amesema kamati yake ina jukumu la kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira rafiki bila maambukizi mapya ya ukimwi na kwamba changamoto yoyote inayokwamisha utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo lazima zitafutiwe ufumbuzi.
Mratibu wa Baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi mkoa wa Mwanza Veronica Joseph amesema NACOPHA inatekeleza mradi wa sauti yetu katika kata kumi za halmashauri ya jiji la Mwanza, kwa lengo la kuongeza ushiriki wa watu wanaoishi na VVU katika shughuli za mwitikio wa ukimwi na kuhamashisha upatikanaji wa matumizi ya huduma rafiki za ukimwi kwa kuimarisha mfumo wa rufaa na taarifa.
ConversionConversion EmoticonEmoticon