vurugu za ibuka katika baraza la madiwani Arusha


Vurugu zimeibuka katika Halmashauri ya jiji la  Arusha cha kufuatia madiwani Wa Chadema kususia na kutoka nje ya ukumbi katika Tukio la kuapishwa kwa madiwani wapya wawili wa waliochaguliwa kupitia chama cha Mapinduzi.

Tukio hilo limetokea baada ya Mkurugenz wa jiji Athmani Kihamia kusoma agenda ya kuapishwa kwa madiwani hao ambapo madiwani wa chadema walitoka nje na badaye kutaka kurejea kitendo kulichotafsriwa na wafuasi wa Ccm waliofika kushuhudia kuwa ni kujaribu kuvuruga tukio la kuapishwa kwa madiwani hao na hivyo Vurugu zikakaanza.

Mkurugenz Wa jiji la Arusha alijaribu kutuliza Vurugu hizo huku akiwataka madiwani waliotoka nje kuendelea kubaki nje lakini hakukuwa na maelewano baina yao kutokana na kelele hizo.

Naye Meya Kalist Lazaro alisimama wakati wa Vurugu hizo kwa kuwa yeye hakuwa miongoni mwa waliotoka nje na naibu Meya wake ambapo aligonga nyundo mezani kutuliza vurugu hizo lakini waliendelea kupigana mpaka askari walipoingilia kati.

Awali akifungua mkutano wa baraza LA madiwani Meya wa jiji amesema kumekuwa na maendeleo katika jiji kutokana na ushirikiano uliopo kati ha madiwani watendaji pamoja na Serikali hivyo kuwataka madiwani wapya na wazamani kuendeleza ushirikiano ili kutekeleza miradi kwa ufanisi.

Hata hivyo malumbano hayo hayakusababisha kikao cha baraza LA madiwani kusimama na mpaka sasa bado baraza linaendelea
Previous
Next Post »