UCHUMI wa wakulima wa kahawa aina ya Arabica wa Kanda ya Kusini unatarajiwa kupanda mara mbili zaidi katika msimu wa kilimo kwa mwaka 2016/2017, ikiwa watazingatia kanuni bora za kilimo cha kisasa.
Hayo yalielezwa hivi karibuni wilayani hapa na Meneja wa Taasisi ya Utafiti wa Zao la Kahawa Tanzania (Ta- CRI), Kanda ya Kusini, Godbless Shao, katika siku ya mkulima wa kahawa na mazao mengine, iliyofanyika katika kijiji cha Mkinga, Mbinga mkoani Ruvuma.
Shao alisema kwa muda mrefu tangu TaCRI ianze mradi wake kanda hiyo iliyopo katika mikoa ya Njombe, Iringa na Ruvuma, wakulima wamekuwa wakipanda miche bora ya kahawa ya vikonyo kutokana na sifa zake za kipekee ikilinganishwa na aina nyingine ya miche ya kahawa.
Meneja huyo alifafanua kuwa miche ya kahawa ya vikonyo ina ukinzani dhidi ya magonjwa ya kutu ya majani na chulebuni (CBD), magonjwa ambayo yasipodhibitiwa mapema, kwa kawaida huwezi kumkosesha mkulima mazao zaidi ya asilimia 50.
“Lengo la siku hii ya mkulima wa kahawa, ni njia mojawapo ya kuwaleta wakulima pamoja, kubadilishana uzoefu wao kwa wao, katika kushirikishana mafanikio na changamoto mbalimbali kutoka katika mashamba yao wakisaidiwa na maofisa ugani wetu na wa halmashauri ili kuongeza tija katika kilimo chao” alisema Shao.
Kwa mujibu wa Shao, pamoja na mambo mengine, TaCRI huwahamasisha na kuwaelimisha wakulima namna nzuri ya kulima kilimo cha kibiashara cha kahawa, jambo ambalo wakulima wamekuwa wakipokea elimu hiyo kwa faida yao na familia zao.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Ofisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya ya Mbinga, Yohanes Nyoni aliwataka wakulima hao, kuzingatia kanuni za kilimo bora cha zao hilo.

ConversionConversion EmoticonEmoticon