MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Rage ameushauri uongozi wa Simba kuhakikisha fedha ambazo klabu hiyo imepata kwa kumuuza mshambuliaji Emmanuel Okwi klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia zinatumika kwa maendeleo ya klabu na si kulipa madeni.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Rage alisema ameambiwa fedha hizo tayari zimeshatumwa kwa klabu hiyo, hivyo ni jukumu la uongozi kuhakikisha masuala ya kimaendeleo yanapatikana.
Alisema dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 600 za Tanzania) ambazo Simba imepewa kwa kumuuza Okwi ni nyingi kama zikitumika vizuri na kwamba kama zikitumiwa vibaya si fedha nyingi.
Pia Rage amesema Simba imepewa dola za Marekani 19,000 (karibu Sh milioni 40) kama riba kutokana na kuchelewa kupewa fedha karibu miaka mitatu sasa na kushauri viongozi wahakikishe wanazitumia vizuri na si kuelekeza katika malipo ya madeni.
“Klabu ina changamoto nyingi za kufanya, sitaki kusema wafanye kitu gani, lakini Simba ina mambo mengi ya maendeleo waelekeze huko, hata kujenga sehemu ambapo wachezaji watakuwa wanaweka kambi yao ” alisema Rage na kuongeza kuwa anashukuru kusikia fedha hizo zimepatikana kwani wapo baadhi ya watu walikuwa wakimshutumu kwamba amekula fedha hizo. “Nilipigania sana hizo fedha wengine wakawa wananishutumu. Naamini sasa kile nilichokuwa nakifanya kimepatikana na nataka kiinufaishe Simba na si kuambiwa zimelipia madeni ya klabu,” alisema.
Akizungumzia suala hilo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema atalizungumzia wakati wowote kuanzia leo.
“Nitaitisha mkutano na waandishi katika siku mbili hizi, nitafafanua mambo mengi,” alisema Manara.
Okwi aliuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia miaka mitatu iliyopita, ambapo Etoile haikulipa fedha hizo Simba na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa mshahara wake kwa miezi mitatu.
Okwi akawafungulia Etoile kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake. Hivi sasa Okwi anacheza soka nchini Denmark.

ConversionConversion EmoticonEmoticon