Je vitu hivi ni vya abiria wa ndege ya MH370 ?

Wanaharakati wamezichapisha picha za vitu vinavyoaminika kuwa mali ya abiria waliokuwa ndani ya ile ndege iliyotoweka ikiwa angani ya Malaysia Air nambari MH370.
Vitu hivyo vilipatikana ufukweni huko Madagascar.
Image captionVitu hivyo vilipatikana ufukweni huko Madagascar.
Vitu hivyo vinajumuisha kibeti, kipochi, na mfuko wa kubebea laptop....vyote vilipatikana na raia mmoja wa Marekani ambaye amekuwa miongoni mwa wapelelezi wanaotafuta ilikotowekea ndege hiyo.
Image captionJamaa ya abiria walioangamia katika ndege hiyo wameombwa kuvitambua vifaa hivyo vya kibinafsi
Sasa jamaa ya abiria walioangamia katika ndege hiyo wameombwa kuvitambua vifaa hivyo vya kibinafsi pamoja na baadhi ya picha zilizopatikana, ili kuweza kubaini ikiwa ni vya jamaa zao.
Image copyrightIBSON
Image captionNdege hiyo iliyokuwa ikitokea Kuala Lumpur ikielekea Beijing- Uchina ilitoweka na abiria wote 210 mnamo mwaka 2014.
Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Kuala Lumpur ikielekea Beijing- Uchina ilitoweka na abiria wote 210 mnamo mwaka 2014
Previous
Next Post »