Mchezaji kiungo wa Switzerland Xherdan Shaqiri amezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii kwa kuikejeli kampuni ya kutengeneza bidhaa za michezo ya Puma kufuatia kupasuka kwa jezi za wachezaji kadhaa wanaoshiriki dimba la Euro2016.
Shaqiri alitahamaki baada ya jezi za wachezaji wanne wa timu ya Uswisi Admir Mehmedi, Breel Embolo, Blerim Dzemaili na Granit Xhaka kukamilisha mechi dhidi ya Ufaransa wakiwa migongo wazi.
Kampuni hiyo ya Ujerumani ililazimika kuomba radhi huku ikidai kuwa kulikuwa na hitilafu wakati wa kutengenezwa kwa jezi za timu hiyo.
Mchezaji aliyesajiliwa majuzi wa Arsenali Xhaka alimaliza mechi hiyo akiwa amebadilisha shati mara tatu.
Lakini hayo yote ni Kennda, Shaqiri alipokuwa akihojiwa na runinga moja ya Uswisi SRF alidondosha mstari unaonukuliwa na maelfu ya mashabiki wake kote duniani.
''natumai Puma hawatenezi kondomu''
Mshambulizi wa zamani Uingereza Gary Lineker alikejeli ubora wa jezi hizo za timu ya Uswisi kwenye mtandao wake wa Twitter.
“Tsheti za Puma za wachezaji wa Uswisi zinapasuka kama karatasi''.
''Mpira wa Adidas unapasuka katikati ya mechi''.
''Je utaamini vipi tena ubora wa bidhaa zinazotokea Ujerumani''
Puma ilijitetea katika taarifa kwa vyombo vya habari ikisema kuwa kati ya mechi 10 za Euro 2016 ambapo jezi zao zilitumika, ni mechi moja iliyodhihirisha hali hii.
''uchunguzi wetu umebaini kuwa jezi 7 zilipasuka uwanjani.
''uchunguzi wa awali pia umebaini kuwa jora iliyokatwa wakati jezi hiyo ya uswisi ikishonwa ilikuwa na hitilafu katika mitambo yetu huko Uturuki.
''Tunaomba radhi na hilo halitatokea tena.'' taarifa hiyo ya puma ilisema.
Mbali na Uswisi, Puma imezipa jezi timu za Austria, jamhuri ya Czech , Italia na Slovakia.
Matukio hayo yanawadia siku chache tu baada ya mpinzani wa Puma Adidas kutangaza kuwa wametia sahihi zabuni ya kuivisha timu ya taifa ya Ujerumani hadi mwaka wa 2022.
Kandarasi hiyo ni ya thamani ya dola milioni 56.5$.
ConversionConversion EmoticonEmoticon