Thamani ya pesa ya Nigeria yashuka dhidi ya dola ya Marekani

Nigeria imeruhusu thamani ya sarafu yake kuyumba katika hatua za kuzuia kuwepo ukosefu wa sarafu za kigeni. Kutokana na hatua hiyo thamani ya naria ilishuka mara moja kwa asilimia 23.
Muda mfupi baada ya kuanza kwa biashara leo Jumatatu, thamani ya naira ilikuwa ni naira 255 kwa dola moja ya Marekani.
Thamani ambayo ilikuwepo awali ilikuwa ni naira 197 kwa dola.
Wachanganuzi wanasema kuwa kushuka kwa bei ya mafuta, imesabasia thamani ya naira kushuka.
Bei ya naira katika masoko yasiyo halali ni 350 kwa dola moja ya Marekani.
Previous
Next Post »