Mwijage: Tanzania inaingia kwenye uchumi wa viwanda



WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Tanzania inaingia kwenye uchumi wa viwanda ili kuwawezesha vijana wengi zaidi kupata ajira.
Alisema hayo juzi wakati wakati akifungua Maonesho ya 13 ya Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) Kanda ya Kaskazini, yanayofanyika katika viwanja wa Mashujaa Mjini hapa.
Mwijage alisema Serikali ya Awamu ya Tano, imedhamiria kujenga viwanda vingi zaidi hasa mahali ambapo pana malighafi za kutosha.
“Serikali ya Magufuli ni ya viwanda, dhima ya miaka mitano ni kujenga uchumi wa viwanda utakaochochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa maisha ya wananchi,” alisema.
Alisema kwa sasa serikali itatengeneza ajira kwa sababu taifa ni changa huku asilimia 65 ya watu wake ni vijana, ambao wengi wao wana umri usiozidi miaka 35 wanahitaji ajira.
“Viwanda vitachochea soko la mazao ya wakulima kwani kwa kupitia viwanda kila atakayejishughulisha atatajirika kwa maana atapata fedha na kipato,” alisema.
Alisema lengo lingine la kuingia uchumi wa viwanda ni kutengeneza bidhaa kwa ajili ya mahitaji ya watu na bidhaa hizo zitauzwa ndani na nje ya nchi. Mwijage alisema wakati huu ni muhimu kuangalia nafasi ya Sido, kwani viwanda vingi ni vile vidogo na vya kati.
Aliwataka maofisa biashara kuwa makocha katika kuelekeza, kwani lengo ni kuhakikisha Sido inakuwa na nguvu.
Alisema sasa wanakwenda kuifufua Sido yenye nguvu, kama iliyokuwa wakati wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambapo ilikuwa na nguvu, tofauti na sasa. Mkurugenzi Mkuu wa Sido, Omar Bakari alisema shirika hilo, linaendelea kubuni mbinu mbalimbali kulingana na mahitaji
Previous
Next Post »