Maafisa 4 wa polisi washtakiwa kwa mauaji Kenya

Maafisa 4 wa polisi wa kituo cha Syokimau Kenya wanaotuhumiwa kwa mauaji ya wakili mmoja na mteja wake pamoja na dereva wao wa teksi wamekanusha mashtaka dhidi yao.
Maafisa hao sajini wa polisi wa utawala Fredrick Leliman,na Leonard Maina Mwangi, pamoja na koplo wa polisi Stephen Chebulet na konstebo Silvia Wanjiku Wanjohi, wamekanusha mashtaka 3 ya mauaji walipofikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Milimani jaji Jessy Lesit.
Upande wa mashtaka umesema kuwa unaandaa mashahidi 45 dhidi ya wanne hao ambao walitibua maandamano ya juma zima mjini Nairobi mawakili wakisusia kazi kufuatia mauaji ya wakili mwenza Willie Kimani,mteja wake Josephat Mwenda na dereva wao wa teksi Joseph Muiruri .
Image copyright
Image captionWakili Willie Kimani
Maafisa hao wa polisi sasa watasalia rumande kwa mwezi mzima.
Maafisa hao wanatuhumiwa kuwateka nyara Wakili Wille na mteja wake walipokuwa wanatoka mahakamani kusikizwa kwa kesi dhidi ya afisa wa polisi aliyempiga risasi mteja wake bila kosa lolote.
Tukio hilo lilitokea mjini Mavoko viungani mwa mji wa Nairobi.
Upande wa mashtaka unasema kuwa baadhi ya mashahidi wao wanalindwa na polisi baada ya kuzuka hofu ya mauaji zaidi yanayotekelezwa na washiriki wa washtakiwa.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 16 mwezi Agosti.
Previous
Next Post »