Riek Machar aondoka Juba na jeshi lake

Makamu wa rais wa Sudan Kusini bwana Riek Machar ameondoka mji mkuu wa Juba, akiandamana na wafuasi wake na jeshi lake.
Msemaji wake bwana James Gatdet Dak ameaiambia shirika la habari la Reuters kuwa bwana Machar ameondoka mjini Juba ilikupunguza uwezekano wa makabiliano na maafa zaidi.
''Imetubidi kundoka Juba ilikujiepusha na purukushani'' Dak ambaye yuko mjini Nairobi kenya aliiambia Reuters.
Hata hivyo amesema kuwa anaendelea kuwasiliana na jeshi tiifu kwa makamu wa rais Riek Machar.
''hata hivyo yuko tu katika sehemu fulani hukohuko Juba''
Image copyrightREUTERS
Image captionRais Salva Kiir na makamu wake bw Machar walitangaza amri ya kusitisha mapigano baina ya wanajeshi watiifu kwao.
''Siwezi kukwaelezeni wapi haswa kwa sababu ya usalama wake''
Rais Salva Kiir na makamu wake bw Machar walitangaza amri ya kusitisha mapigano baina ya wanajeshi watiifu kwao.
Hata hivyo kufikia wakati huo watu zaidi ya 270 walikuwa wamekwishapoteza maisha yao tangu mapigano hayo yatokee Alhamisi juma lililopita.
Previous
Next Post »