Tetekuwanga ni ugonjwa unasababishwa na
virusi viitwavyo Varicel Zoster. Ugonjwa huu una ambukizwa kwa haraka sana.
Vipele hufanana na malengelenge; na vinawasha sana. Ugonjwa huu ni wa hatari
zaidi kwa watoto wachanga,watu wazima na wale ambao kinga ya mwili imeshuka.
Dalili
Vipele vya ugonjwa huu huanzia kwenye
kiwiliwili na usoni kisha kuenea mwili mzima. Vipele vinafanana na lengelenge,
vinawasha kisha huacha kovu. Makovu ya ugonjwa huu si ya kudumu kwani baada ya
muda hufifia.
Dalili nyingine ambazo hujitokeza siku moja
au mbili kabla ya vipele ni
-homa kali
-uchovu
-kukosa hamu ya kula
-maumivu ya kichwa
Maambukizi
Ugonjwa huu husambaa kwa njia ya hewa pale
mgonjwa anapopiga chafya au kupenga. Pia huweza kusambaa endapo endapo
utakugasana na majimaji yenye virusi toka kwa mgonjwa. Mgonjwa huanza
kuambukiza kabla vipele havijatoka na huendelea kuambukiza mpaka makovu
yanapotoka.
Ukiugua ugonjwa huu mara moja unaweza kupata
kinga ya kudumu. Mtu aliyewahi kuugua tetekuwanga anaweza kuugua mkanda wa
jeshi.
Kinga.
Unaweza kujikinga na ugonjwa huu iwapo
utapata chanjo. Katika nchi zilizoendelea chanjo za ugonjwa huu hutolewa kwa
watoto wote.
Matibabu
Kwa kawaida ugonjwa huu hauitaji dawa lakini
kama dawa ikianzishwa ndani ya masaa 24 huleta manufaa na hupunguza dalili za
ugonjwa kwa kiasi kikubwa. Matibabu makubwa hulenga kudhibiti dalili kam homa,
mwili kuwasha na upungufu wa maji mwilini.
Hata hivyo watu wenye upungufu wa kinga,
wanaotumia dawa za kushusha kinga, saratani ya ngozi, wajawazito wanahitaji
uangalizi maalumu.
TETEKUWANGA:
Ugonjwa wa
tetekuwanga husababishwa na vijidudu vidogo sana aina ya vijasumu. huanza wiki
2 hadi 3 baada ya mtoto kukaa na mtoto mwingine ambaye tayari anao ugonjwa huu.
Kwanza kabisa,
madoadoa au vipele vidogo sana vyekundu na ambavyo huwasha, huanza kutokea.
Hivi, hubadilika
na kuwa malengelenge na mwishowe, kufanya ganga vyote kwa wakati mmoja.
Kawaida huanza
kwenye mwili na baadaye hutokea kwenye uso, mikono na miguu.
Kunaweza kukawa
na vipele, malengelenge, na ganga vyote kwa wakati mmoja. Kwa kawaida homa ni
kidogo tu.
Tiba:
Ugonjwa hupona baada ya wiki moja. Ukoge kila siku kwa sabuni
na maji ya uvuguvugu ili kupunguza kuwasha. Tumia nguo baridi zilizoloweshwa kwenye
maji yaliyotokana na shayiri iliyochemshwa na kukamuliwa.
Kata kucha za mikono ziwe fupi kabisa. Kama ganga zinapata
ugonjwa, paka gentia violet (g.v) au mafuta ya kuua vijidudu.
Utatuzi wa kiasili wa tetekuwanga ni pamoja na maji ya pea,
magadi ya kuoka , mafuta ya vitamini E , asali, chai mitishamba au karoti na
korianda. Inaaminika kwamba muwasho wa ngozi unaweza kupunguzwa kwa
kiwango fulani kwa maji ambayo yametumika kupikia mbaazi
mabichi. Losheni inayotengenezwa kwa magadi ya kuoka na maji yanaweza kuwekwa
kwenye ngozi za wagonjwa kwa sponji ili kupunguza mwasho. Pia, kupaka
mafuta ya vitamini E au asali kwa ngozi
hudhaniwa kuwa na athari ya uponyaji kwa alama ambazo zinaweza kubakia baada ya
maambukizi kutibiwa. Baadhi ya watu wanadai kuwa athari za kutuliza kwa kadri
za chai ya
kijani zina ufanisi wa kupunguza dalili.
ConversionConversion EmoticonEmoticon