Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imeanza zoezi la kubomoa nyumba zinazojengwa katikati ya mji bila kufuata taratibu za ujenzi zinazotolewa na Manispaa hiyo.
Zoezi hilo limekuja kufuatia baadhi ya wananchi waliopewa vibali vya ukarabati na Manispaa hiyo kugeuza matumizi ya vibali hivyo na kuvitumia katika ujenzi.
Akiongoza utekelezaji wa zoezi hilo, Mkuu wa oparesheni Ally Bera amesema zoezi hili ni endelevu ili kuhakikisha hakuna ujenzi holela utaofanyika katika manispaa hiyo.
Bera ametoa rai kwa yeyote anayetaka kujenga katika Manispaa ya Dodoma kuhakikisha ana kibali cha ujenzi.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia ubomoaji wameunga mkono zoezi hilo na kutaka liwe la endelevu.
ConversionConversion EmoticonEmoticon