Miaka 30 jela kwa kumkatisha mtoto wa kike masomo na kumuozesha


Baba mlezi wa mwanafunzi mmoja wa darasa la pili wilayani Same mkoani Kilimanjaro amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlazimisha mtoto huyo kukatisha masomo na kuolewa.
Akizungumzia tukio hilo Afisa ustawi wa jamii wilayani Same, Lucy Venance amesema baadhi ya wazazi wamekuwa mstari wa mbele kukwamisha jitihada za watoto wao kuendelea na masomo.
Katika kipindi cha mwaka 2017, Halmashauri ya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imepokea matukio manne ya watoto wa kike kutaka kuozeshwa ambapo watuhumiwa watatu walitoroshwa licha ya watoto waliofanyiwa ukatili huo kuokolewa.
Kituo cha Ushauri Same ambacho kinamhudumia mwanafunzi huyo kwa sasa kimeitaka jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu na kutimiza ndoto zao.
mwandishi wetu ilizungumza na Mwendesha mashtaka katika mahakama ya wilaya ya Same, Ancibetus Kechoka ambaye amekiri kupokea shtaka hilo ambapo mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka thelathini huku katibu tawala wa wilaya ya Same, Sospeter Magonera akielezea azma ya kuendelea kuwatafuta wazazi wa mtoto huyo.
Previous
Next Post »