Rais Dkt. John Magufuli amehoji gharama za kuwasafirisha na kuwakimu baadhi ya majaji na familia zao wanaokwenda likizo nje ya nchi.
Rais Magufuli amesema hayo wakati akihutubia katika kilele cha wiki ya sheria jijini Dar es salaam ambapo amesema anaujua vema mshahara wa majaji na hivyo kuhoji uwezo wao kuishi nje ya nchi kwa siku 28 za likizo.
“Baadhi ya majaji wanaenda likizo nje ya nchi kama vile Afrika kusini na Uingereza na wanakwenda na familia zao kwa siku zote 28 nilikuuliza Jaji Mkuu ukakosa majibu, nataka tume yako ifanyie kazi jambo hili” amesema Rais Magufuli.
Kadhalika Rais amesema anashangazwa kwa nini kanuni za msaada wa sheria za mwaka 2017 zimeshindikana kusainiwa na kumtaka Waziri wa Katiba na Sheria kukamilisha kanuni hizo ndani ya siku 28.
Sambamba na hayo Rais Dkt. Magufuli amewataka watendaji wa mahakama kutenda haki katika kazi zao na serikali itawaunga mkono kwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.
ConversionConversion EmoticonEmoticon