Akizungumza Mwenyekiti UWT mkoa wa Arusha Jasmini Bachu amesema kuwa katika eneo la Kaloleni kuna Jumla ya maduka 72 ambayo yanalipiwa shilingi milioni 6 laki tatu na 10 na Eneo la Levolosi kuna Maduka 72 ambayo yanalipiwa milioni 6 laki 3 na nusu Fedha ambazo haziendani na thamani ya maduka hayo.
Bachu amesema kuwa eneo hilo la Kaloleni kila duka linalipiwa shilingi elfu 80 na Kaloleni Kila mpangaji analipa laki moja na kuna watu wameingia mikataba na wafanyabiashara na kuwalipa wao na UWT ndo walipwe kodi zao jambo ambalo amesema ni kinyume cha Utaratibu.
Amesema kuwa kinachofanyika ni uzembe na upotevu wa Mali za jumuiya ya UWT ameomba mkaguzi wa mahesabu wa Mali za jumuiya hiyo kuanza kuchunguza kwa kuwa kilichokuwa kinafanyika Fedha nilikuwa zinapitia mikononi mwa watu na siyo banki kama utaratibu wa malipo ulivyo.
Bachu amesikitika kuona watu wachache wanafaidi na kufanya wananchi kuichukia Serikali yao ambapo amesema hatakubali na wote waliofanya hivyo mamlaka husika itafuatilia na
Amegiza wafanyabiashara wote kulipia kodi benki na kuacha Mara moja kulipa Fedha mkononi.
Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Arusha Fatuma Hassani ameonekana kuwa na wasiwasi wakati wa kuhakiki maduka hayo amekuwa akiwafundisha wafanyabiashara kumjibu Mwenyekiti wa UWT jambo lilosababisha sintofahamu.
Mmoja wa mfanyabiashara ambaye hakutaja Jina lake litajwe amesema kuwa kinachofanywa ni wizi na rushwa kwasababu yeye anamlipa aliyempangishia duka shilingi laki 2,50000 lakini UWT wanapata shilingi 80000 ambapo amemshukuru Mwenyekiti huyo kwa ujasiri wa kubaini Mali za jumuiya hiyo.
"Hakiamungu Mimi huyu mama nimempenda bure na ndiyo majembe ya Raisi yani tunanyonywa mno sasa Si bora tupangishiwe sisi tulipe moja kwa moja huko UWT kuliko kulipa laki mbili kwa hawa watu kumbe wezi tu wanapeleka 80000"Amesema
Kamati hiyo imeongozwa na wajumbe 8 akiwemo Anna Msuya Mjumbe wa baraza kuu UWT Taifa,Agnes Martin, Asha Saidi,Asha Mohammed, Felister Nanyaro,Christina Bayo,Jofa Kakani , Fatuma Hasani Katibu UWT Mkoa,Pamoja na Mwenyekiti UWT Jasmini Bachu.
ConversionConversion EmoticonEmoticon