Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanzia ziara ya siku tano Mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amesema pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais atazindua miradi ya afya, elimu na kuzungumza na wananchi.
Hii ni mara ya pili kwa Makamu wa Rais kufanya ziara Mkoani Iringa ambapo mwaka jana alifika mkoani humo kuzindua kikosi kazi cha kunusuru mto Ruaha Mkuu.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Makamu wa Rais.
ConversionConversion EmoticonEmoticon