Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati ya kutosha itakayowezesha pamba yote inayolimwa nchini kununuliwa na tayari imeshaanza mchakato wa kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni Mjini Dodoma.
Amesema mwishoni mwa mwaka jana serikali iliwaita wakuu wa mikoa, wakurugenzi na wakuu wa wilaya ambao walipewa maelekezo ya kwenda kuhamasisha kilimo cha zao hilo na kuwasaidia wakulima kuanzia ngazi ya awali.
Amesema serikali inashiriki kikamilifu katika usimamizi wa zao la Pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba kwa kulima kitaalam, upatikanaji wa pembejeo hadi utafutaji wa masoko.
Kuhusu soko la nje, Waziri Mkuu amesema Wizara ya Kilimo inawasiliana na mataifa mbalimbali ili kuhakikisha pamba yote iliyolimwa nchini inanunuliwa.
ConversionConversion EmoticonEmoticon