Wazazi na Walezi zingatieni mtindo ya nywele kwa watoto wadogo

Nikweli watoto wanatakiwa kupendeza kuanzia mavazi hadi nywele zao zinatakiwa kua safi na nadhifu. Lakini ni mitindo gani? sio kila mtindo mtoto anatakiwa asukwe mingine ni ya kikubwa sana unamkomaza tu mtoto iepuke. Kwa mfano mtoto chini ya miaka 10 amesukwa yeboyebo kubwa na marangi ya rasta mengi kichwa hii sio sahihi jamani. Watoto wakike wanamisuko yao ya kitoto na wanapendeza wakisukwa. Au kumsuka hii mitindo ya sikuizi wanaita crochet mtoto anakua na kichwa kikubwa kwa sababu ya ukubwa wa nywele hiyo pia sio sahihi na haipendezi tuwaachie wakubwa.
Misuko mingine unamkaza mtoto kichwa mwishowe anaanza kuumwa kichwa, kuota vidonda na vipele na mara nyingine hadi wanazimia sio vizuri na ni dhambi. Mtoto asuke mtindo unaendana na umri wake. Vivyo hivyo kwa watoto wa kiume wanyoe mitindo ya kuendana na umri na vichwa vyao.
Previous
Next Post »