Waziri azindua kampeni ya kuchangia vifaa vya kujifunzia mashuleni


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ametoa rai kwa jamii kuunga mkono mpango wa serikali wa kutoa elimu bure kwa kujitolea vifaa vya kujifunzia ili kuwezesha wanafunzi wanaotoka katika familia zenye uhitaji kupata elimu.
Waziri Jafo ametoa rai hiyo wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kusaidia Vifaa vya Kujifunzia kwa watoto wanaotoka katika familia zisizo na uwezo, uliofanyika katika shule ya msingi Uguzi wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Mpango huo unaiitwa “NISAIDIE DAFTARI NA PENI NAMI NIPATE ELIMU”.
Naye Kaimu Afisa Elimu wilaya ya Chamwino Abraham Msigwa amesisitiza suala la kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya elimu, katika kuwezesha wanafunzi namna ya kujifunza huku baadhi ya wanafunzi wakikiri kuwa vifaa vya kujifunzia ni changamoto kwa baadhi yao.
Previous
Next Post »