WIZARA YA MAJI NCHINI TANZANIA IKO KWENYE MCHAKATO WA KUANZISHA WAKALA WA MAJI VIJIJINI


WIZARA ya Maji na Umwagiliaji ipo iko kwenye mchakato wa kuanzisha Wakala wa Maji Vijijini ili kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali vijijini.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isaac Kamwele alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni, (CCM) aliyetaka kujua wizara ina mkakati gani ili kuharakisha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini.
Kamwelwe alisema, tayari wizara hiyo ilishaunda Mfuko wa Maji ambao hadi sasa una takribani Sh milioni 158, lakini kwa sasa mkakati wa wizara hiyo ni kuhakikisha inaunda Wakala wa Maji Vijijini ili kusaidia katika kampeni ya usambazaji wa maji vijijini kama ilivyo kwa Wakala wa Barabara wa Vijijini (TARURA).
Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Bukoba, Jasson Rweikiza (CCM) aliyetaka kujua, ni kwanini serikali haichukui hatua kusaidia wananchi wa maeneo ya vijijini hasa katika Wilaya ya Bukoba Vijijini, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Josephat Kakunda alisema serikali inachukua hatua kuboresha huduma za maji. Alisema, kupitia Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa mwaka 2018/2019, serikali imetenga Sh bilioni 2.9 kwa ajili ya uboreshaji huduma za maji.
Previous
Next Post »