WATU WATATU WAFARIKI DUNIA MKOANI SINGIDA KWA KULA CHAKULA KINACHOSADIKIKA NI SUMU


Watu wanne wamefariki dunia katika kijiji cha Kintinku, wilaya ya Manyoni mkoani Singida katika  matukio mawili tofauti yaliyotokea wilayani humo likiwemo la watu watatu wa familia moja kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Manyoni, Ainea Mlewa amethibitisha kutokea kwa matukio hayo likiwemo la mwanamke mmoja kupoteza maisha wakati akipatiwa matibabu baada ya kaka yake kumkata kata kwa panga.
Matukio hayo yemevuta hisia za watu wengi ambao walikusanyika katika hospitali ya wilaya ya Manyoni  wakati miili ya watu hao ikichukuliwa kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti .
Kwa mujibu wa mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Manyoni,watu hao watatu waliokufa baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu wawili ni wanafunzi wa shule ya msingi Lusilile iliyoko wilayani Manyoni.
Tayari sampuli za chakula walichokula zimechukuliwa  kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha vifo vya watu hao.
Katika tukio la pili mwanamke alikatwa kwa panga na kaka yake na  kulazwa katika hospitali hiyo ya manyoni ambapo alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.
Previous
Next Post »